1 / 30

Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka!

UCHAMBUZI WA VIUMBE Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! www.bionet-intl.org | bionet@bionet-intl.org Mchanganuo huu umekusanywa na BioNET (Posa Skelton & Kornelia Rassmann) kwa ushirikiano na wafwatao UTANGULIZI Henrik Enghoff Natural History Museum of Denmark

benjamin
Download Presentation

Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka!

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. UCHAMBUZI WA VIUMBE Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! www.bionet-intl.org | bionet@bionet-intl.org Mchanganuo huu umekusanywa na BioNET (Posa Skelton & Kornelia Rassmann) kwa ushirikiano na wafwatao UTANGULIZI Henrik EnghoffNatural History Museum of Denmark Ulf GärdenforsArtDatabanken, Swedish Species Information Centre Fabian HaasAfrican Insect Science for Food and Health Chris LyalNatural History Museum, London Yves SamynRoyal Belgian Institute of Natural Sciences Ensifera ensifera (Boissonneau, 1840)Mchoraji: Ernst Haeckel Kiswahili: Melckzedeck K. M. Osore, Western Indian Ocean Marine Science Association (WIOMSA)

  2. MIMI NI NANI? UTANGULIZI Je, unatakakujua? Muulizemchambuziwaviumbe Au bonyeza Kiunganishi hiki … © Stuart Wynne

  3. Neno Taxonomy asili yake ni maneno mawili ya kigiriki: Taxis = mgao/mpangilio, nomos = Sheria Kugundua Kutoa jina Kueleza Kuainisha UCHAMBUZI WA VIUMBE NI …Sayansi ya viumbe UCHAMBUZI WA VIUMBE NI Ili kuelewa bioanuai (na mengine yanayohusu…)

  4. KUGUNDUA Ugunduzi wa viumbe wapya ndio hatua ya kwanza ya uchambuzi wa viumbe. Kila mwaka viumbe wapya wanagunduliwa kote ulimwenguni, kadri wachambuzi wanapo tembelea maeneo mapya, au vinapopatikana vitendea kazi vipya vya kuchambua sampuli UCHAMBUZI WA VIUMBE NI Samaki aina ya Dracula (Dracula fish) Danionella draculaAmegunduliwa nchini Burma Ameelezewa 2009 © Ralf Britz | Natural History Museum, London

  5. KUTOA JINA Electrolux addisoni (Compagno & Heemstra, 2007) Jina lina muundo gani? Jina la kisayansi ni hati inayo tambulisha viumbe wote UCHAMBUZI WA VIUMBE NI Photo: Phil Heemstra | Wikimedia Commons Sio fagio lako la kawaida!

  6. KUELEZEA Sehemu ya mchakato huu inahusu kulinganisha viumbe wanao husiana karibu ili kuthibitisha kama kiumbe fulani ni wa aina mpya. UCHAMBUZI WA VIUMBE NI Hypsiboas calcaratus (Troschel, 1848) | Photo: P. J. R. Kok

  7. UAINISHAJI Jina langu ni Dolly! Kingdom - Animalia Phylum - Chordata Class - Mammalia Infraclass - Eutheria Order - Artiodactyla Family - Bovidae Subfamily - Caprinae Genus - Ovis Species - Ovis aries UCHAMBUZI WA VIUMBE NI

  8. UAINISHAJIni muhimu katika maisha yako ya kila siku Uainishaji ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Hutuwezesha kupanga vitu katika utaratibu unaofaa kama uhakiki mali katika (Supermarket) maduka makubwa. Je, unategemea kuzipata bidhaa za maziwa zimeorodheshwa pembeni mwa zile za usafi wa nyumbani? MAJINA NI MUHIMU Photo: G. R. South

  9. MAJINAni muhimu katika maisha yako ya kila siku ? Drawing: Peter Aertsen Photo: Sergio Kaminski | Wikimedia commons MAJINA NI MUHIMU Hebu fikiria kama yasingekuwepo majina ya watu na vitu… Photo: Wikimedia commons | public domain

  10. MAJINAyanahitajika kwa mawasiliano Panya Muis Ratón • Majina ya kawaida au ya lugha za asili ni muhimu kwa mawasiliano ya kila siku lakini matumizi yake ni finyu kutegemea mahali na lugha マウス فأس Ποντίκι MAJINA NI MUHIMU Souris 쥐 Мышь Mouse Mus Maus 老鼠 © Kornelia Rassmann

  11. MAJINA YA KISAYANSIkwa mawasiliano kimataifa Alternanthera philoxeroides Bursaphelenchus xylophilus MAJINA NI MUHIMU Photo: L.D. DwinellUSDA Forest Service, United States | forestryimages.org Photo: Gary BuckinghamUSDA Agricultural Research Service, United States | forestryimages.org Pseudophilotes sinaicus • Kutumia jina la kisayansi ni hakikisho kwamba tunazungumza kuhusu kiumbe fulani bila pingamizi kutokana na eneo letu kijiografia au lugha Photo: BioNET-NAFRINET

  12. KulijuaJINA SAHIHI- kunaokoa fedha MAJINA NI MUHIMU Photo: Oliver Spalt | Wikimedia commons Scotinophara luridaPhoto: Natasha Wright, Florida Department of Agriculture and Consumer Services, Bugwood.org • Elimu ya uchambuzi imesaidia kubaini aina ya kombamwiko weusi 24 tofauti inchini Ufilipino, na kati ya hao ni 2 pekee ndiyo waharibifu walioshambulia mchele. Ujuzi huu anaokoa mamilioni ya dola katika matumizi ya viuwa tilifu vya wadudu kwa kuwadhibiti na husaidia kulinda mazingira. • See case study no. 39

  13. KUTOJUA JINA- kunaweza kuua! MAJINA NI MUHIMU Boletus aurantiacus | Photo: Wikimedia commons | public domain Nile au nisile? Muulizemchambuziwauyoga (mycologist)!

  14. LINNAEUS "Ikiwa hauyajui majina ya vitu, ni kazi bure kuelewa umuhimu wa vitu hivyo" Critica Botanica 1737 MAJINA NI MUHIMU Carl von Linné(au Linnaeus), ndiye “babawauchambuziwaviumbe”, yeyendiyealiyewekamsingiwamfumowakisasawamajina – wakuwapaviumbemajinakisayansi. Carl von Linné, 1707-1778 Drawing: AMNH Library Linnaeus ndiye alieanzisha uainishaji thabiti na sahihi unaohitajika kuieleza bioanuwai, bidhaa za biashara, ununuzi wa mbegu za ukulima, udhibiti wa wadudu waharibifu, au ushughulikiaji wa aina nyingine ya maeneo mengi yanayohitaji ujuzi wa uchambuzi wa viumbe.

  15. UMUHIMU NA UHUSIANO NABIOANUWAI © A. De Kesel Uelewa wa uchambuzi wa viumbe una manufaa kwa sekta nyingi zinazoshirikiana kufanya kazi moja kwa moja au kwa namna mbalimbali na bioanuwai. Ikiwa unajihusisha na biashara ya kuigiza na kutoa bidhaa inchini, uhakiki wa chakula, madawa, afya ya jamii, mabadiliko ya tabia inchi, usalama wa viumbe, kilimo, kilimo cha bustani, uvuvi, sayansi ya mifugo, madini, utalii, au hata kazi za jikoni, masuala ya sekta hizi zote yanahitaji elimu ya dunia hai. UCHAMBUZI - MANUFAA Uelewa wa uchambuzi wa viumbe unatuwezesha kuelewa uanuwai wetu wa viumbe.

  16. UFAHAMU WA DUNIA HAI © Kornelia Rassmann Utofauti wa viumbe mbali mbali unafanya dunia yetu iwe ya utata. Uelewa wauchambuzi wa viumbeunasaidia kufahamu huu utofauti kwa njia ya kupanga na kwa kuuweka ulimwengu wetu katika makundi yanayo eleweka vizuri. UCHAMBUZI - MANUFAA

  17. UCHAMBUZI WA VIUMBEmanufaa kwa ustawi wa binadamu Huleta uelewa wa msingi katika maeneo mbali mabli ya manufaa kwa mwanadamu yakiwemo uhifadhi wa bioanuwai, kukabiliana na madadiliko ya tabia nchi, usalama wa viumbe , ukulima,ufugaji samaki, afya, utalii, biashara na mengine mengi. UCHAMBUZI - MANUFAA Photo: Bigstockphoto.com Photo: ??? Photo: Posa A. Skelton

  18. UCHAMBUZI WA VIUMBE ni Swala muhimu kimataifa Husaidia katika maamuzi mema ya sera na udhibiti, hutoa muongozo katika huduma za msingi (kwa mfano katika ukulima, dawa) na ni msingi wa miundombinu ya Malengo ya Milennia yanayohusu kupunguza umaskini, kupambana na magonjwa na kuendeleza mazingira. UCHAMBUZI - MANUFAA © Kornelia Rassmann

  19. MSINGI WA ELIMU kwa sayansi nyingine Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia maeneo mbalimbali ya kisayansi pamoja na sayansi ya hifadhi, biolojia ya uzinduzi, biologia ya uvumbuzi, ikolojia, biojiografia, dawa na mengine mengi. UCHAMBUZI - MANUFAA Photo: G. R. South Photo: BioNET-MESOAMERINET

  20. Uhifadhi wa BIOANUWAI Kwa kutambua bioanuwai zetu tunaweza kuzihifadhi na kuzitumia kwa uendelevu. Kwa mfano: Hifadhi mbalimbali zimeanzishwa kwa sababu ya kugundulika kuwa maeneo ya viumbe hadimuni au maeneo hayo kutambulika kuwa makazi ya viumbe waliodhaniwa kuwa wameshatoweka. UCHAMBUZI - MANUFAA © Posa A. Skelton Brachylophus bulabula – aina mpya ya Iguana(aina ya mjusi mkubwa sana) anaye patikana tu katika nchi ya Fiji.

  21. TABIA NCHI kukabiliana na mabadiliko Kusambaa kwa viumbe kutaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi. Maktaba ya viumbe huchangia pakubwa kuhifadhi kumbukumbu za kudumu za kihistoria jinsi viumbe wa aina mbali mbali walivyo sambaa, na kutoa fursa nzuri ya kutabiri uwezekano wa viumbe hao kutoweka, kuenea kwa wadudu waharibifu na maambukizi ya magonjwa na kusaidia katika hatua za kukabiliana na mazingira. UCHAMBUZI - MANUFAA © Gert Brovad

  22. VIUMBE WAVAMIZI & WADUDU WAHARIBIFU Usimamizi mzuri UtumiziwakombamwikowaainayaCyrtobagoussalviniaekudhibitikueneakwagugumajimkubwawaainayaSalviniamolesta. Viumbe wavamizi huathiri karibu kila aina ya mazingira duniani na ni tishio kubwa kwa bioanuai. Ili kuepukana na hathari hizi, wachambuzi wa viumbe wenye uzoefu na vifaa vya kutosha wanahitajika kutoa taarifa upesi na kutambua haraka aina na vifaa muhimu vinavyohitajika kutumiwa na viongozi na wanajamii. UCHAMBUZI - MANUFAA Photo: Katherine Parys, Louisiana State University, United States • See case study no. 27

  23. SERA / MAAMUZI Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuratibu sera na mfumo wa muongozo. Kwa mfano: Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia Kuangamia (CITES ), hutegemea taarifa sahihi za uchambuzi kufanikisha udhibiti mzuri wa biashara ya aina ya viumbe hao, kama vile orchids (aina ya mmea wa maua). Viumbe wanaoorodheshwa na Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia Kuangamia (ujulikanao kama CITES) hulindwa kwa viwango na aina tofauti dhidi ya matumizi holela. UCHAMBUZI - MANUFAA Karibu aina zote za mimea hii zimeorodheshwa na CITES, idadi kubwa katika Kiambatanisho cha pili (appendix II) ambacho kinajumuisha aina ambazo sasa hazitishiwi na kuangamia lakini zinaweza kuan-gamia kama biashara haitadhibitiwa kwa makini. © Martin Voggenreiterclockwise: Ophrys fusca, Orchis italica, Cypripedium calceolus, Ophrys lutea

  24. UGUNDUZI WA VIUMBE HAI & AFYA © Posa Skelton - Morinda citrifolia © Stuart Wynne - Niphates digitalis Mimea yenye dawa ni muhimu katika sehemu nyingi duniani, na uchambuzi wa viumbe hutumika kutambua mimea yenye manufaa, kama vile tunda la Noni. UCHAMBUZI - MANUFAA Sifongo wa baharini (marine sponges) ni chanzo kizuri cha misombo ya muhimu kwa kutengeneza madawa, viungo vya chakula na vifaa vingine kwa matumizi ya kibiashara. Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia kugundua na kubainisha haya.

  25. For a similar case study see case study no. 8 UHAKIKA WA VIUMBE HAI & BIASHARA Mdudu asiye fahamika anapopatikana katika shehena ya kilimo, anaweza kusababisha kupungua kwa kasi ya biashara duniani na shehena husika inaweza kucheleweshwa kwa muda mrefu na gharama kubwa ikisubiri mdudu huyo atambuliwe barabara. Katika hali hii, uelewa wa uchambuzi wa viumbe unaweza kuokoa fedha. UCHAMBUZI - MANUFAA Madai ya kuwepo kwa aina fulani ya mba (anaye julikana kama Karnal bunt fungus) katika shehena ya ngano toka nchi ya Australia kulisababisha kukataliwa kwa shehena hiyo kuingia nchini Pakistan. Kwa kutumia uchambuzi wa viumbe, ilibainika kwamba chembechembe zilikua sio za mba husika ambao hutambulika kwa kuvamia maeneo. Kutatuliwa kwa swala hilo kulizuia kusitishwa kwa biashara ya ngano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni nne. Tilletia indica|Photo: Ruben Durán, Washington State University, Bugwood.org

  26. KUPUNGUZA UMASKINI&UHAKIKA WA CHAKULA Kupunguza umaskini, uhakika wa chakula na uhifadhi wa viumbe hai huenda sambamba. Kimataifa, umaskini na uhaba wa chakula mara nyingi hupatikana sehemu zilizopoteza idadi kubwa ya viumbe hai. Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuendeleza mazingira yenye afya katika nchi zinazoendelea, ambapo hupatikana kiwango kikubwa cha bioanuai duniani, lakini pia idadi kubwa ya watu wa kipato cha chini vijijini wakitishiwa na upungufu wa bioanuai. UCHAMBUZI - MANUFAA © bluerain | Dreamstime.de © imagedirekt.de

  27. UCHAMBUZI WA VIUMBE:kuendeleza elimu yetu Hadi sasa, aina takriban milioni 1.8 wamegundu-liwa. Inakisiwa yakwamba idadi kamili ni kati ya milioni 5 hadi 50. Tafakari mfano huu: Katika utafiti uliyohusisha kiumbe aitwaye cricket (anayefana kama panzi) wa nchini Australia, asilimia 76 ya viumbe hao waligundu-liwa kuwa wapya. From Otte, D., and R. D. Alexander. 1983. The Australian Crickets (Orthoptera: Gryllidae). Academy of Natural Sciences of Philadelphia. Viumbe wapatao 18,500 wa aina impya waligunduliwa mwaka 2007 CHANGAMOTO Unka boreena (Otte & Alexander) | Photo: David Rentz

  28. UKUBWA tu wa KUKUMBATIWA Sio hoja Uchambuzi unahusu sio tu viumbe wenye karama wanaojulikana na kila mtu, kama vile Nyangumi, na wanyama wengine wakubwa wanaoishi nje ya Afrika kama Giant Panda, na Polar bear (aina ya dubu). CHANGAMOTO © Tatiana Goydenko | Dreamstime.com Unahusu pia viumbe wadogo wanaosababisha mazingira yetu kustawi. Baadhi ya viumbe hawa wadogo wadogo wanaweza kutufaa maishani mwetu (mfano chachu) ama kutuathiri (mfano mbu anaye eneza malaria)! © Josef Szasz–Fabian | Dreamstime.com

  29. DUNIA ina SHANGAZA Hippocampus satomiae | © Rudie Kuiter © John Sear Sayari yetu ina maajabu mengi ya kushangaza na hazina nyingi – viumbe wapya hugunduliwa kila siku lakini mwanadamu (Homo sapiens kwa jina la kisayansi) haupi ugunduzi huu thamani inavyostahili. Kiumbe huyu aitwaye Seahorse (mwenye umbile la farasi mdogo sana anayeishi baharini) aliyegunduliwa rasmi mwaka 2008 ndiye mnyama mdogo sana wa aina yake. Ana urefu wa 13.8 mm na kimo chake ni takriban 11.5mm. CHANGAMOTO

  30. Una hamu ya kujua mengi kuhusuUCHAMBUZI WA VIUMBE? Hapa utapata maelezo zaidi kuhusu... Uchambuzi wa viumbe Global Taxonomy Initiative (GTI, UN Convention of Biological Diversity)| European Distributed Institute of Taxonomy (EDIT) |Natural History Museum, London, UK) |Royal Belgian Institute of Natural Sciences | BioNET-International Aina ya viumbe Encyclopedia of Life (EoL) |Wikispecies | ARKive |IUCN Red List |Top 10 New Species Discoveries International Institute for Species Exploration (IIES) | Tree of Life | Census of Marine Life (CoML) | Catalogue of Life (ITIS, Species2000) | Global Biodiversity Information Facility (GBIF) Umuhimu wa uchambuzi, aina ya viumbe & bioanuai BioNET case studies |GTI case study on taxonomy & climate change | UN Convention of Biodiversity – 2010 International Year of Biodiversity MAELEZO Photos: BioNET-SAFRINET, BioNET ANDINONET, BioNET-EAFRINET, BioNET-NAFRINET

More Related