1 / 2

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA III. AFYA NA MADAWA

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA III. AFYA NA MADAWA. Kemia imechangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya viumbe hasa katika nyanja za afya na madawa ambapo imetupelekea kuishi maisha marefu, ya furaha na afya.

genero
Download Presentation

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA III. AFYA NA MADAWA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIAIII. AFYA NA MADAWA Kemia imechangia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya viumbe hasa katika nyanja za afya na madawa ambapo imetupelekea kuishi maisha marefu, ya furaha na afya. Katika kipindi kirefu cha historia ya mwanadamu, masuala ya tiba na afya yalikuwa ni ya kizamani. Ikitokezea mtu kuumwa ama kupata ajali wakati huo madaktari pamoja na jitihada walizokuwa wakizichukua walishindwa kuwaridhisha moja kwa moja wagonjwa wao katika tiba hizo. Karibu miaka 100 iliyopita sekta ya afya imekuwa na mabadiliko makubwa kwa madaktari kuweza kuponya wagonjwa kwa kutibu maradhi kwa uhakika zaidi, kutibu majeraha na hata kuweza kukinga matatizo makubwa ya afya kabla hayajatokea. Jitihada kubwa za wakemia pamoja na wahandisi kemikali wamefanikiwa kugundua dawa za kisasa baada ya kuendeleza mawazo mapya ya wafamasia, kuvumbua vifaa vya kisasa vya kutengenezea madawa pamoja na kuboreshwa mbinu za kuchunguza maradhi. Maisha ya mamilioni ya binaadamu yameokolewa, huduma za afya, tiba na madawa zimeimarishwa kutokana na maendeleo ya kemia. III.1. Udhibiti wa Maumivu, Maumivu Makali na Uvimbe (Pain and Inflammation Management) Morphine Aspirini Cortisone III.2. Udhibiti wa Magonjwa ya Akili (Psychotherapeutic Agents) Chlorpromazine Tricyclic antidepressants Benzodiazepines III.3. Homoni na Kirekebishi Homoni (Hormones and Hormone Regulators) Insulini Testosterone Progestins, estrojeni, na dawa za uzazi wa mpangilio (oral contraceptives) III.4. Udhibiti wa Matatizo ya Tumbo (Gastro-intestinal Agents) Uvumbuzi wa tiba za vidonda vya tumbo (ulcer) III.5. Uchunguzi wa Afya na Magonjwa (Medical Testing and DiseaseDiagnostics) Teknolojia za tiba Isotopu (isotopes) za tiba Maendeleo ya upimaji ubora wa kemikali Uvumbuzi wa kujichunguza afya III.6. Dawa za Kuzuia Maambukizi (Anti-infective Drugs) Salvarsan naProntosil Penicillin Zidovudine (AZT) III.7. Uangalizi wa Mishipa ya Moyo (Cardiovascular Management) Kurekebisha mapigo ya moyo Tiba ya moyo kushindwa kufanya kazi Athari za kuganda kwa damu Kudhibiti kiwango cha kolestroli katika damu III.8. Tibakemikali ya Saratani (Cancer Chemotherapy) Kuvumbuliwa kwa tibakemikali (kemotherapi) ya saratani Dawa aina ya cytotoxic. Tamoxifen III.9. Vifaa vya Matunzo ya Afya (Novel Healthcare Materials) Viungo bandia na vifaa vya tiba Zana za tiba mbali mbali Dawa wa kuulia vijidudu na dawa za kuondosha madoa

  2. III. MATOKEO MUHIMU YA TEKNOLOJIA KATIKA AFYA NA MADAWA Matukio: 1899 Aspirin yavumbuliwa kupambana na maumivu, maumivu makali ya viungo pamoja na uvimbe. 1909Salvarsan tiba kuu kemikali ya kwanza kuanzishwa. 1922Insulin yaanza kutumika kuondosha kiwango kikubwa cha sukari katika damu ambayo huchangia ugonjwa wa kisukari. 1923Muundo kemikali wa Morphine wagunduliwa. 1927Kipima mimba kimeboreshwa ili kuweza kugundua estrojeni katika mkojo. 1935Prontosil hutibu maambukizi hatari yanayosababishwa na bakteria wa streptococcal. 1942Nitrojeni yaanza kutumika kama tibakemikali pekee ya ugonjwa wa saratani. 1943Penicillin yatibu maambukizi na yazinduliwa kama dawa ya kutibu vijisumu. 1954Digoxin yathibitishwa kuwa tiba ya magonjwa ya mgando kwa damu katika moyo (mfumo wa mgando wa damu). 1954Chlorpromazine yaanza kutumika kama tiba ya kisasa ya magonjwa ya akili. 1960Enovid yatengenezwa na kuanza kuuzwa kama dawa za uzazi wa mpangilio. 1963Herbal Cytotoxic dawa itumikayo kutibu saratani 1976Tagamet huzuia kuenea kwa tindikali ndani ya tumbo wakati wa tiba ya vidonda vya tumbo. 1977Tamoxifen huzuia homoni katika tibakemikali (kemotherapi) ya saratani. 1987Zidovudine (AZT) imethibitishwa na FDA kutibu maambukizi ya HIV. Aspirin, dawa ya kwanza kutengenezwa (1900) Paul Ehrlich, mvumbuzi wa Salvarsan Frederick Banting na Charles H. Best wagunduzi wa insulini. Muundo kemikali wa Morphine Kipima mimba Prontosil Utaratibu kazi wa penicilin. Picha ya Alexander Fleming katika dirisha la kioo Muundo kemikali wa Taxol, ni dawa aina ya cytotoxic. ENOVID Upindo wa rangi ya waridi huashiria mapambano dhidi ya saratani ya matiti, upindo mwekundu huashiria mapambano dhidi ya UKIMWI Vidonda vya tumbo

More Related