270 likes | 483 Views
MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA. Uliofanyika Mwanza Juni 10, 2008. Utangulizi. Mwanza una wilaya nane -Geita -Sengerema -Kwimba -Ukerewe -Misungwi -Magu -Nyamagana -Ilemela. Utangulizi. Eneo la kilometa za mraba 35,187 Kilometa za mraba 15,092 (43%) ni maji
E N D
MDAHALAO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI WA MKOA WA MWANZA Uliofanyika Mwanza Juni 10, 2008
Utangulizi • Mwanza una wilaya nane -Geita -Sengerema -Kwimba -Ukerewe -Misungwi -Magu -Nyamagana -Ilemela
Utangulizi • Eneo la kilometa za mraba 35,187 • Kilometa za mraba 15,092 (43%) ni maji • Shughuli kubwa za kiuchumi ni -Kilimo -Ufugaji -Uvuvi -Uchimbaji madini • Idadi ya watu ni milioni 3.5
Hali ya Uchumi na Umaskini • Pato la mkoa ni sh. milioni 961,672 (nafasi ya 2 kitaifa) • Pato la mkoa la kila mtu ni sh. 309,577 (nafasi ya 12 kitaifa) • Kiwango cha umaskini ni 48.33% (nafasi ya 18 kitaifa)
Matokeo Kutokana na Ripoti za Wilaya • Maeneo 9 ya kupewa kipaumbele katika uwezeshaji wa kiuchumi katika mkoa wa Mwanza. -Kilimo -Uvuvi -Ufugaji -Biashara na viwanda
Matokeo Kutokana na Ripoti za Wilaya -Madini -Utalii -Nishati -Misitu -Taasisi za fedha na mitaji
Kilimo • Fursa -Hali ya hewa nzuri • Matatizo -Uhaba wa ardhi -Utegemezi kwa mvua, -Tija ndogo kwenye kilimo -Bei ndogo ya mazao
Kilimo Mikakati • Wilaya zipangiwe mazao mawili ya kulima kutokana na ubora wa mazingira yake badala ya kila wilaya kulima mazao yote • Kuboresha na kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo na kuwa na mashamba darasa ili kuongeza tija • Kuanzishwa kwa kilimo cha alizeti
Kilimo • Kuanzisha maghala ya kijiji • Kushawishi serikali kuu iwekeze kwenye maghala ya kisasa ya wilaya • Kuanzisha kilimo cha majaluba karibu na ziwa Viktoria • Kuboresha uelimishaji wa wakulima wadogo ili kuboresha tija kwenye kilimo • Kuwezesha watu wachache wenye uwezo ili wafanye ukulima wa kisasa
Uvuvi • Fursa -Nguvukazi ya uvuvi • Vikwazo -Uvuvi usio endelevu -Usalama majini
Uvuvi Mikakati • Kuboresha taarifa za masoko na bei ya samaki. • Kuhamasisha uanzishwaji wa mabwawa ya kufuga sato ili kufanya uvuvi uwe endelevu. • Kuboresha usimamizi wa serikali kwenye sekta ya uvuvi ili wavuvi wasionewe kibei.
Uvuvi • Kuanzisha minada ya samaki ili iwe sehemu pekee ya kuuza na kununua samaki ili kusaidia wavuvi kupata bei nzuri. • Ujenzi wa mabwawa ya kuzuia maji ili kuwezesha ufugaji samaki. • Kuongeza bidii kudhibiti uvuvi haramu
Ufugaji • Fursa -Uwepo wa mifugo mingi • Kikwazo -Ubora duni wa mifugo kitija
Ufugaji Mikakati • Kuboresha aina ya ng’ombe kwa kufanya “breeding” ili kupata ng’ombe wakubwa zaidi wenye kutoa ngozi, nyama na maziwa zaidi. • Kuelimisha wakulima juu ya faida ya kubadilisha aina ya ng’ombe.
Ufugaji • Serikali kuu isaidie kuboresha kituo cha Mabuki. • Kuanzishwa kwa ufugaji wa mbuni na mamba kwa ajili ya kuuza bidhaa zake kibiashara. • Ufugaji wa wanyamapori katika zoo ili kuvutia watalii
Biashara na Viwanda • Fursa -Nguvukazi • Kikwazo -Upatikanaji mgumu wa mikopo
Biashara na Viwanda Mikakati • Serikali itoe guarantee ya mikopo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati. • Kuhamasisha serikali kupunguza idadi ya wadhibiti ili kupunguza gharama za kufanya biashara. • Kuhamasisha wafanyabiashara kuongeza thamani kwenye bidhaa wanazonunua kabla ya kuuza.
Biashara na Viwanda • Kuwajengea wamachinga mijini sehemu moja ya kufanyia biashara. • Kuhamasisha serikali kuu, kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Mwanza kwa kuwapunguzia gharama za kufanya biashara. • Kuhamasisha serikali kabadili mfumo wa sheria ili kuiachia sekta binafsi kufanya shughuli zake ili kuinyanyua sekta binafsi
Madini • Fursa -Wingi wa madini • Kikwazo -Mitaji midogo ya wachimbaji wadogo.
Madini Mkakati • Kuwawezesha wachimabaji wadogo wawezeshwe kwa njia ya soko, vifaa na utafiti wawezeshwe kwa kupitia SACCOs.
Misitu • Fursa -Hali ya hewa inayoruhusu kuota kwa miti ya aina mbalimbali • Kikwazo -Kupungua kwa miti
Misitu Mikakati • Kuelimisha watu juu ya faida za kufuga nyuki wa asali kwa njia ya vikundi. • Kupanda miti kama mitiki na misandale kwa ajili ya kuuza nje na kuwezesha upatikanaji wa mkaa.
Utalii • Fursa -Kuwepo sehemu za kitalii Mwanza na ukaribu wa mkoa na sehemu za kitalii • Kikwazo • Kutokufahamika sehemu za kitalii vizuri
Utalii Mikakati • Kuhamasisha watalii wanaokwenda Serengeti kupitia Mwanza. • Kuhamasisha watu binafsi wawekeze kwenye marestaurant. • Kuandika nakala kuhusu historia ya mkoa na kuitawanya ili kuboresha ufahamu wa watu wa sehemu za kihistoria za mkoa. • Kuandika ripoti ya fursa za kitalii za mkoa wa Mwanza.
Nishati • Kikwazo ni uhaba wa nishati umeme Mikakati • Kuvutia wawekezaji wa nishati ya umeme Mwanza. • Kuhamasisha utumiaji umeme wa jua, umeme wa wanyama kazi na dizeli vijijini.
Taasisi za Fedha na Mitaji • Kikwazo ni ugumu wa taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo kutokana na kutokuwa na imani nao
Taasisi za Fedha na Mitaji Mikakati • Kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOs • Uboreshaji wa SACCOs • Kuwapa mafunzo wafanyabiashara wadogo ili kuzifanya taasisi za kifedha ziwe na imani nao. • Kuanzisha benki ya wananchi ambayo wanahisa wakubwa ni SACCOs.