1 / 27

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA. Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam. DONDOO. Usuli Utangulizi Mafanikio Changamoto Masuala ya Mjadala. 1.0. USULI.

cain-flores
Download Presentation

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam.

  2. DONDOO • Usuli • Utangulizi • Mafanikio • Changamoto • Masuala ya Mjadala

  3. 1.0. USULI • MKUKUTA unatekelezwa kupitia michakato ya serikali, Programme za mageuzi/maboresho na programu za maendeleo za kisekta • Hatua zinazochukuliwa na asasi zisizo za kiserikali (Sekta binafsi, mashirika ya hiari, vyama vya wafanyakazi, taasisi za kidini) • Hivyo, Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA imeandaliwa kutokana na taarifa za utekelezaji za wadau hawa.

  4. 2.0. UTANGULIZI • Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA (2007/8) inatoa sura ya jumla ya mafanikio, changamoto, mambo tuliyojifunza na hatua zinazofuata katika kutekeleza nguzo zote tatu za MKUKUTA • Hatua zilizofikiwa katika • Ugharimiaji, ufuatiliaji na tathmini • Michakato na mageuzi na jinsi hatua hizi zilivyochangia kufikiwa kwa matokeo ya MKUKUTA • Taarifa hii imezingatia uwepo wa Taarifa za Utekelezaji za MDAs na za wadau wasio wa kiserikali

  5. …Inaendelea • Taarifa hizi zinatoa hatua zilizochukuliwa na mafanikio kwa kina zaidi • Kwa maeneo fulani takwimu hazijabadilika sana ikilinganishwa na taarifa ya 2006/7 • Aidha katika baadhi ya maeneo takwimu za karibuni hazikupatikana hasa zile zinazotokana na savei. • Taarifa hii imejikita zaidi katika kipindi cha hadi Juni 2008 • Lengo kuu la Ripoti hii ni kutoa taarifa ya hatua zilizofikiwa na kuamsha majadiliano kwa ajili ya kuboresha hatua zinazofuata.

  6. 3.0. MAFANIKIO: Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato • Serikali imeendelea kutekeleza sera, mikakati na mageuzi kwa lengo la kuimarisha uchumi • Viashiria vingi vinaonyesha mwelekeo mzuri • Mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 7.3 (2006) hadi 7.0 (2007) ingawa ni juu ya lengo la MKUKUTA la asilimia 5 • Makusanyo ya kodi kama asilimia ya pato la taifa yameongezeka • Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka katika mwaka 2007/8 • Deni la taifa limeongezeka lakini endelevu • Thamani ya uwekezaji kutoka nje imeongezeka • Ajira mpya 437,205 zimepatikana • Pato la taifa limeongezeka na hivyo pato la wastani la mwananchi

  7. 2.2. Ubora wa Maisha na Ustawi wa Jamii • Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kuboresha maisha na ustawi wa jamii • Elimu – utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu umeendelea kutoa mafanikio mazuri • Elimu ya Awali • Idadi ya watoto walioandikishwa (Net) imeongezeka kutoka asilimia 33.1 hadi 36.2 Gross kutoka asilimia35.2 hadi38.1 mwaka 2008 • Idadi ya watoto wenye ulemavu walioandikishwa imeongezeka kutoka 685 hadi 2146

  8. …Inaendelea • Elimu ya Msingi • Watoto walioandikishwa darasa la kwanza (Net) imefikia asilimia 97.2 • Wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari imefikia asilimia 56.7 • Watoto yatima walioandikishwa wameongezeka kutoka 748,641 (2007) hadi 915,234 (2008) • Watoto wenye ulemavu walioandikishwa wameongezeka kutoka 24,003 (2007) hadi 34,661(2008)

  9. …Inaendelea • Elimu ya Sekondari • Wanafunzi wanaoingia sekondari (NER) imefikia asilimia 23.5. Lengo la MKUKUTA ni asilimia 25 kufikia mwaka 2010 • Elimu ya Juu • Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu wamefikia 75,346 (wasichana ni asilimia 35)

  10. …Inaendelea • Afya • Programu mbalimbali zimeendelea kutekelezwa katika sekta ya Afya chini ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) • Elimu ya kinga • Kampeni za chanjo • Kuzuia maambukizo • Pamekuwa na mafanikio kadha katika eneo la afya ya mtoto na mama • Watoto waliochanjwa wakati wa kuzaliwa wamefikia asilimia 73 • Wagonjwa wa malaria wameendelea kupungua na hivyo kupelekea kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano • Hata hivyo kumekuwa na tofauti ya matokeo haya kati ya mijini na vijijini • Chanjo ya surua imefikia asilimia 85 • Vifo vya kinamama bado viko juu (hakuna takwimu mpya)

  11. …Inaendelea • VVU/UKIMWI • Juhudi zimeendelea kufanyika kupambana na UKIMWI chini ya Tume ya UKIMWI na Programu ya kudhibiti UKIMWI (NACP) • Usimamizi wa mambukizo yanayotokana na zinaa • Kupima na ushauri nasaha wa UKIMWI • Kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto • Asilimia 47 ya mama wajawazito walipata huduma ya kupima UKIMWI kwenye vituo vya PMTCT kufikia Desemba 2007 • Asilimia 34 ya wliopatikana na VVU walipatiwa dawa ya ARV kuzuia maambukizi kwa mtoto

  12. …Inaendelea • Sekta ya Maji • Serikali imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji • Maji vijijini • Maji mijini • Maji taka • Kumekuwepo na ongezeko dogo ya idadi ya watu wanaopata maji safi na salama vijijini • Takwimu za savei zinaonyesha kuwa pamekuwa na kupungua kwa asilimia ya wanaopata maji safi na salama • Hali ni mbaya zaidi kwa upande wa jiji la Dar Es Salaam

  13. …Inaendelea • Kinga ya Jamii • Serikali inakamilisha mwongozo wa kinga ya jamii kwa ajili ya kuyashughulikia makundi yaliyo katika hatari ya kuathirika zaidi na umaskini • Katika mwaka 2007/8 serikali imeendelea kusaidia makundi yenye mahitaji maalum • Serikali imeendelea kuhudumia makazi 17 ya wazee • Imeendelea kuhudumia vyuo vitatu vya mafunzo (Vocational training colleges) kwa ajili ya watu wenye ulemavu • Serikali imesaidia mafunzo ya stadi watoto yatima 270 walio katika vituo vya kuwalelea (Remands and rehabilitation centres)

  14. 2.3. Governance and Accountability • Serikali imeendelea kutekeleza Mwongozo wa Utawala Bora • Maeneo muhimu ya mwongozo ni pamoja na • Ushiriki wa wananchi katika maamuzi yahusuyo maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi • Sekta binafsi na mwongozo wa udhibiti • Katiba, utawala wa sheria, usimamizi wa haki na kinga ya haki za binadamu

  15. …Inaendelea • Usawa wa jinsia • Uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika usimamizi wa masuala umma • Demokrasia ya uchaguzi na • Utumishi wa umma

  16. …Inaendelea • Hatua za kuridhisha zimefikiwa katika utekelezaji wa mwongozo • Serikali imepitia sheria 12 katika kipindi cha 2007/08 • Miswada 34 iliandaliwa ambapo miswada 23 ilipitishwa kuwa sheria • Serikali pia ilianzisha tovuti kwa ajili ya kupokea maoni/malalamiko ya wananchi

  17. …Inaendelea • Serikali imeendelea kutekeleza utaratibu wa kupeleka madaraka zaidi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (D by D) ili kuwa na utoaji bora wa huduma kwa umma • Wizara 14 zilitathminiwa ili kuona jinsi zinavyotekeleza na kuboresha utaratibu huu • Mchakato huu umeboresha matumizi ya fedha zilizopokelewa na LGAs • Mchakato pia umeongeza uwazi katika kutenga fedha na usahihi wa fedha zilizotegwa kwa shughuli mbalimbali

  18. …Inaendelea • Vita dhidi ya rushwa iliendelea katika mwaka 2007/8 • Tuhuma 2,887 zilichunguzwa ambapo uchunguzi wa tuhuma 1009 ulikamilika • Kesi … zimefikishwa mahakamani katika mwaka 2007/8 • Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuboresha utumishi wa umma • Mapitio ya sera ya malipo ya muda wa kati • Kuajiri watumishi wapya 36,331 kutoka vyuo vikuu

  19. …Inaendelea • Hatua pia zimeendelea kuchukuliwa kuimarisha uwezo mahakama • Kuongeza bajeti ya sekta • Ongezeko la Majaji wa Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa • Juhudi za kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa zimeendelea kuimarishwa • Kuongezwa kwa uwezo wa mabweni ya wafungwa magerezani • Kuboresha usafiri wa watuhumiwa wakati wa kesi zao

  20. 2.4. Ugharimiaji wa MKUKUTA • MKUKUTA unatekelezwa na wadau wote, hivyo na ugharimiaji wake • Serikali imekuwa ikitekeleza MKUKUTA kupitia bajeti yake kila mwaka • Mwongozo wa Mipango na Bajeti umeendelea kuhimiza utengwaji wa fedha kwa kuzingatia vipaumbele vya MKUKUTA • Katika mwaka 2007/8 asilimia 62.7 ya bajeti ilielekezwa kwenye vipaumbele vya MKUKUTA • Asilimia 49.37 (Nguzo ya I) • Asilimia 29.48 (Nguzo ya II) • Asilimia 21.15 (Nguzo ya II)

  21. 2.5. UFUATILIAJI NA TATHMINI • Shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya MKUKUTA imeendelea kutekelezwa kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, Mifumo ya Ufuatiliaji wa MDAs na ule Mamlaka za Serikali za Mitaa • Mfumo wa kitaasisi wa Ufuatiliaji (Kamati na Vikundi kazi) vimeendelea kutekeleza mipango yao ya kazi za ufuatiliaji wa MKUKUTA

  22. …Inaendelea • Katika mwaka 2007/8 Mfumo umetoa taarifa mbalimbali • Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu – 2007 • Ripoti ya Tathmini ya Utoaji Huduma Nchini • Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA • Kijarida cha MKUKUTA (Electronic) • Ushauri wa kisera • Aidha tafiti na savei mbalimbali zilifanyika • Mapato na Matumizi ya Kaya 2007

  23. 3.0. CHANGAMOTO • Changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa nguzo ya I • Kupanda kwa bei za petroli • Kutokuwa na nishati ya umeme yenye uhakika • Uwezo mdogo wa kutumia fedha za matengenezo ya barabara • Masuala ya manunuzi katika eneo la barabara (Procurement capacity, timing, planning etc) • Kutokuwa na utaratibu wa mikopo ya muda mrefu katika kilimo

  24. …Inaendelea • Changamoto katika utekelezaji wa ubora wa maisha na ustawi wa jamii zinahusiana na • Masuala ya ubora wa huduma • Upatikanaji na gharama za huduma • Masuala ya rasilimali watu (Waalimu na Wauguzi) • Ongezeko la watu hasa makundi maalum (watoto yatima, watu wenye ulemavu, wazee) • Masuala ya manunuzi • Rasilimali fedha

  25. …Inaendelea • Baadhi ya changamoto katika utawala bora na uwajibikaji ni pamoja na • Usimamizi na uratibu wa mageuzi hasa katika kupeleka majukumu kwenye Halmashauri na kupeleka wataalam • Kujenga uwezo wa halmashauri kumudu majukumu yanayohamishiwa • Utaratibu wa manunuzi unakwamisha

  26. 4.0. MASUALA YA MJADALA • Haya ni baadhi ya masuala yanayohitaji kupata maelezo sahihi ili kuchukua hatua zitakazosaidia kurebisha au kuongeza kasi • Lengo ni kuwezesha kuanzisha mijadala katika michakato ya kisera na mipango iliyopo ili kuboresha hatua zinazochukuliwa • Baadhi ya masuala ni pamoja na • Ukuaji endelevu wa uchumi na kupungua kwa umaskini • Kilimo cha kisasa na kupunguza umaskini

  27. …Inaendelea • Nishati • Nishati mbadala • Nishati ya mimea na uhakika wa chakula • Elimu na Mkakati wa Kukuza Uchumi • Masuala ya idadi ya watu

More Related