1 / 32

TAARIFA YA ZIARA YA KUJIFUNZA MFUMO WA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA WILAYANI IGUNGA

TAARIFA YA ZIARA YA KUJIFUNZA MFUMO WA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA WILAYANI IGUNGA. WAJUMBE WA TIMU: Timu ya Wataalam waliofanya ziara ya kujifunza mambo mbalimbali wilayani Igunga ni:- Kulwijila, N. S. – Mshauri wa Kilimo Kija Maheda – Mshauri wa Ushirika

denton
Download Presentation

TAARIFA YA ZIARA YA KUJIFUNZA MFUMO WA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA WILAYANI IGUNGA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. TAARIFA YA ZIARA YA KUJIFUNZA MFUMO WA UNUNUZI WA ZAO LA PAMBA WILAYANI IGUNGA

  2. WAJUMBE WA TIMU: • Timu ya Wataalam waliofanya ziara ya kujifunza mambo mbalimbali wilayani Igunga ni:- • Kulwijila, N. S. – Mshauri wa Kilimo • Kija Maheda – Mshauri wa Ushirika • John Masalu – Meneja Shughuli Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza • Nole Joseph – Mhasibu Msaidizi Chama cha Kikuu cha Ushirika Nyanza • Yusuf Kilimo – Dereva wa gari

  3. Madhumuni ya Ziara • Timu ya Wataalam waliotajwa hapo juu ilifanya ziara ya kujifunza wilayani Igunga • tarehe 14 – 17/4/2008. Madhumuni ya ziara hii ilikuwa ni kujifunza mambo yafuatayo:- - Utaratibu wa Ununuzi wa Pamba • - Kilimo cha Mpunga kwa njia ya Umwagiliaji kwa kutumia bwawa la • Mwamapuli. • - Kilimo cha Alizeti • Viongozi/Watumishi/Wadau waliozumgumza na timu:

  4. Katika kufanikisha ziara hii, timu ilikutana na kuhojiana na Viongozi/Watumishi wafuatao:- • - Mkuu wa Wilaya • - Katibu Tawala (W) • - Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) • - Afisa Kilimo/Mifugo (W) • - Afisa Ushirika (W) • - Afisa Umwagiliaji (W) • - Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembesabo ambae vilevile ni • M/kiti wa wa Chama cha Ushirika cha uzalishaji wa zao la mpunga kwa kutumia • Umwagiliaji unaotokana na maji ya bwawa la Mwamapuli. • - Mkaguzi wa Pamba (W) kutoka Bodi ya Pamba • - Mameneja wa Vyama vya Msingi vya:-

  5. Ilambabuki AMCS Ltd. • - Meneja mradi wa uzalishaji mpunga • - Wanachama/wakulima wa Chama cha Ushirika cha Uzalishaji wa zao la mpunga • waliomo katika mradi. • Tuliyojifunza:

  6. Utaratibu wa ununuzi wa zao la pamba. • Kuhusu eneo hili timu ilipata maelezokama ifuatavyo:- • Uongozi wa wilaya uliweka azimio kuwa, ununuzi wa zao la pamba utafanyika katika Vyama vya Ushirika vya Msingi ambao watakuwa mawakala wa kununmua pamba kwa niaba ya Makampuni husika. • Katika kuhakikisha kuwa utaratibu huu unafuatwa, uongozi wa wilaya pia ulifanya mkutano na watendaji wa vijiji wote, watendaji na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi, Maafisa kilimo vijijini pamoja na wanunuzi kuwaelezea uamuzi wa wilaya. Na kwamba kila mtu kwa nafasi yake auelewe, auzingatie na autekeleze.

  7. Timu iliarifiwa kuwa, utaratibu huu ndio unaotekelezwa wilayani na faida zake ni kama ifuatavyo:- • Kila kijiji kuna Chama cha Ushirika cha Msingi ambacho kina ghala la kuhifadhia mazao ambalo ni imara. Hali hii hufanya uhifadhi wa mazao kuwa mzuri na hivyo kuongeza usafi na ubora wa zao. • Kutokana na ununuzi kufanyika sehemu moja (katika Chama cha msingi) uthibiti wa usafi na ubora wa zao umeimarishwa na kufanya wilaya kuongoza katika ubora wa zao hili kitaifa. • Vyama vya Msingi vinakuwa na uhai kiuchumi kutokana na ushuru vinavyopata kama wakala. • Kwa kuwa na takwimu kuwa sahihi, Halmashauri ya Wilaya inapata ushuru unaostahili

  8. Kwa kuwa na kituo kimoja katika kijiji, pamba huchambuliwa na kutenganishwa katika madaraja kwani mkulima hana nafasi ya kupekeka sehemu nyingine kama pamba yake ni chafu. • Utaratibu huu unapunguza udanganyifu wa kumwibia mkulima kupitia mizani isiyokuwa sahihi. Mizani ya Vyama vya Misingi si rahisi kuirekebisha kwa lengo la kupunguza uzito.

  9. Mkulima hakopwi mazao yake na pale (kituo cha ununuzi) ndipo wanunuzi hushindana kihalali kwani mwenye bei kubwa ndiye hununuliwa pamba kwanza mpaka fedha yake iishe; kila mnunuzi hutangaza bei ya kununulia katika Chama cha Msingi.

  10. Changamoto/matatizo Matatizo na changamoto yanayoukabili utaratibu huu ni kama ifuatavyo:- • Watumishi wa Vyama vya Msingi hawana dhamana ya fedha wanazopokea kutoka kwa wanunuzi bali ni uaminifu tu ndo unaotumika. • Wanachama wa Vyama vya Msingi wanalalamikia viongozi wao kuhusu matumizi yasiyoridhisha ya fedha za ushuru zinazopatikana. • Wanachama wa Vyama vya Msingi wanalalamikia viongozi wao kuhusu matumizi yasiyoridhisha ya fedha za ushuru zinazopatikana.

  11. Kuna tatizo la mizani (Weigh bridge) kwenye jineri. Uzito unaopimwa/kwenye Chama cha Msingi hupungua unapopimwa ngazi ya jineri hivyo Chama cha Msingi hufidia upungufu huo. Wanunuzi huweka Bima kwa pamba yao lakini maghala ambayo ni mali ya Chama cha Msingi hayawekewi Bima.

  12. Ununuzi ngazi ya Chama cha Msingi: - Chama cha msingi kinafunga mkataba na wanunuzi ambapo mkataba husainiwa na • mnunuzi, viongozi wa Chama cha Msingi, Mtendaji wa kijiji na mwisho Hakimu. • - Fumigation hufanywa na wanunuzi • Wanunuzi huleta fedha zao kwenye Chama cha Msingi na kutangaza bei zao. Chama cha Msingi huanza kumnunulia pamba yule aliyetoa bei kubwa, na fedha zake zikiisha ndipo huanza kumnunulia yule ambaye bei yake inafuata.

  13. Mnunuzi huleta gari pindi fedha zake zinapoisha kwa ajili ya kusomba hivyo pamba hairundikani kwenye ghala. • Gharama za kushindilia mazao kwenye magunia na posho ya wajumbe wanaosafirisha pamba – hadi kwenye jineri zinagharimiwa na Chama cha Msingi. • Ushuru wa kuwanunulia wanunuzi ni TSh. 15 kwa kilo.

  14. Changamoto: • Changamoto: • Kutokana na bei tofauti tofauti wakati wa ununuzi, wanunuzi hupendelea kutumia bei ndogo (ya chini) kuonyesha kuwa ndio iliyotumika kununulia kiasi kikubwa (kilo) cha pamba ili waitumie bei hiyo kulipia ushuru mdogo kwa H/Wilaya. • - Maghala hayawekewi bima • - Mikataba inayofungwa haipelekwi kwa Afisa Ushirika ili kuhakikisha kuwa kanuni na taratibu za Ushirika zinafuatwa.

  15. Maoni/Mapendekezo ya Timu

  16. Utaratibu wa ununuzi wa pamba unaotumika wilayani Igunga wa zao kununuliwa • katika kituo kimoja na hasa vyama vya msingi ni mzuri. Rejea faida zilizotajwa. • Kama tunataka kuimarisha usafi na ubora wa pamba ambao ndio umekuwa tatizo kubwa ni vizuri tuige utaratibu huu.

  17. Bila kuzingatia kanuni za kilimo bora cha zao husika uzalishaji wetu utaendelea kuwa mdogo. Suala la kufuata kanuni za kilimo bora katika mradi wa Mwamapuli ni la lazima na mwanachama asiyetekeleza huchukuliwa hatua au kufukuzwa katika mradi. • Ushirikishaji wa Wadau wote wa pamba (Watendaji wa vijiji, viongozi wa vyama vya msingi, maafisa kilimo vijijini na wananunuzi imesaidia wilaya katika kuhakikisha utaratibu wa ununuzi unafuatwa.

  18. Soko ni nyenzo muhimu katika kuiimarisha kilimo cha zao husika. Pamoja na kuwepo kiwanda cha kukamulia mafuta bado kilimo cha zao hili hakijaimarika wilayani Igunga kwani bei ni ndogo (TSh. 100 kwa kilo). Bei hii bado haijawa motisha kwa wakulima wengi kushiriki .

  19. Changamoto ya mkoa: • Mkoa wetu unazalisha kiasi kikubwa cha pamba ikilinganishwa na Wilaya ya Igunga hivyo inatakiwa kuweka mikakati mizuri zaidi kwa kutumia kituo, kimoja cha kununulia Pamba ili kuweza kuboresha zao la Pamba na upatikanaji wa takwimu sahihi za Pamba na kuongeza mapato katika vyama vya Msingi na Halmashauri za Wilaya.

  20. Hitimisho:

  21. Ununuzi wa pamba kwa kutumia kituo kimoja katika kijiji (one buying post) unaweza kutatua matatizo mengi tunayokabiliana nayo kwa sasa. Utaratibu wa ununuzi kwa stakabadhi za mazao ghalani bado haujaanza kutekelezwa Wilayani Igunga. • Naambatanisha baadhi ya vielelezo kwa ajili ya kusaidia ufafanuzi na uelewa zaidi (Kiambatisho Na. 1 – 4).

  22. MAPENDEKEZO YA TIMU YA WATAALAAM • UTANGULIZI: • Utaratibu unaotumika Igunga unawezekana Mkoani kwetu, kwa sababu:- • i. Kila Kijiji kina ghala lakini baadhi ya Maghala yanahitaji ukarabati. • ii. Kila chama cha Msingi kina Bodi ya Chama cha Msingi na Mwandishi • (Katibu Meneja). • iii. Kila chama cha Msingi kina Safe (Kasiki) • iv. Na baadhi ya vyama vya Msingi vina silaha (Bunduki) • v. Waandishi wa vyama vya Msingi wana wadhamini, udhamini unaothibitishwa na Mwenyekiti na Mtendaji wa Kijiji kwa kila Kijiji husika. Kubaini Mali zilizowekwa dhamana kama kweli zipo na wanazimiliki kihalali.

  23. MAPENDEKEZO YA UTARATIBU HUU KUANZA KUTUMIKA: • (i)Tunapendekezo utaratibu huu uanze Msimu huu 2008/2009

  24. ENEO LA KUTUMIKA KWA UTARATIBU HUU: • (i) Tumependekeza wilaya zote za Mkoa huu zianze kutumia utaratibu huu. • UTARATIBU WA UNUNUZI: • (i) Wanunuzi wote kikiwemo Chama Kikuu cha Ushirika watanunulia kituo kimoja (Chama cha Msingi) Mwanunuzi Mwenye bei kubwa ndiye atakayeanza kununuliwa pamba kwanza; pamoja na utaratibu huu kuwa mzuri, tulikuwa tunaomba kwenda Mtwala/Lindi kwa ajiri ya kujifunza utaratibu wa ununuzi wa mazao ya biashara kwa njia ya stakabadhi ya mazao ghalani, ili kuweza kulinganisha taratibu hizo mbili, Lengo ni kuona mkulima ananufaika vipi, ukilinganisha na gharama za uzalishaji.

  25. MNUNUZI. • Mnunuzi atatoa fedha za kununulia pamba pamoja na vitabu vyote vinavyohusiana na ununuzi wa pamba kwa wakala.

  26. Mnunuzi atamlipa WAKALA kamisheni(Agency fee)Tsh.15 kwa kiloya pamba . Mnunuzi atamlipa atalipa kamishini kwa pamba iliyopokelewa kwa wa taratibu za pamba zilizowekwa na mnunuzi. Mnunuzi atatoa bei ya kununulia pamba kwa WAKALA.

  27. MNUNUZI halazimiki kupokea pamba ilyochini ya kiwango cha ubora kama inavyotakiwa na mamlaka inayosimamia ubora wa pamba.

  28. MNUNUZI atasafirisha pamba ilyonunuliwa na WAKALA toka chama cha msingi hadi kiwandani. • WAKALA. • Wakala atatoa ghala lake litumike kununua pamba kwenye chama cha msingi kwa kipndi chote cha ununuzi Wakala atumia mizani na cash box zake. • Wakala atatakiwa kutunza kumbukumbu zote za manunuzi ya pamba. Kumbukumbu hizi zinatakiwa kuandaliwa vizuri na kuwa wazi wakati wote kwa ajili ya ukaguzi endapo zitahitjika. • Wakala atalazimka kuweka ulinzi madhubuti wa mali iliyo ndani y ghala wakati wote wa msimu.

  29. Wakala atalazimika kusindikiza pamba yake inaposafirishwa na mnunuzi kutoka gulioni hadi kiwandani • Wakala atatakiwa kutumia fedha za ununuzi wa pamba kwa kazi iliyokusudiwa tu(ununuzi wa pamba ) na si vinginevyo.Pia wakala haruhusisiwi kuhamisha pamba iliyonunuliwa kwa mnunuzi wingine. • Wakala hatatoa ghala alilotoa kwa ---------litumke kwa kampuni kununulia pamba au kwa matumizi mengine. • Endapo patakuwepo wa mali au fedha ya mnunuzi Wakala (WATUMISHI PAMOJA NA HALMASHAURI) watawajibika na wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

  30. Kiambatisho; Na. 1Rasimu ya mkataba wa ununuzi wa zao la pamba. • MKATABA WA UNUNUZI WA PAMBA MSIMU--------------. • Mkataba huu utakaojulikana kama mkataba wa ununuzi wa pamba msimu-------------umefungwa leo tarehe -------mwezi--------mwaka-------kati ya Kampuni ya -----------------itakayojulikana kama MNUNUZI kwa upande mmoja na CHAMA CHA MSINGI CHA ------------------------S.L.P----------KITAJULIKANA kama WAKALA kwa upande mwingine. • Hivyo inakubalika kwamba WAKALA atanunua pamba toka kwa wakulima kwa niaba ya MNUNUZI kwa masharti na makubaliano yafuatayo;

  31. MNUNUZI. • Mnunuzi atatoa fedha za kununulia pamba pamoja na vitabu vyote vinavyohusiana na ununuzi wa pamba kwa wakala. • Mnunuzi atamlipa WAKALA kamisheni(Agency fee)Tsh.15 kwa kiloya pamba . Mnunuzi atamlipa atalipa kamishini kwa pamba iliyopokelewa kwa wa taratibu za pamba zilizowekwa na mnunuzi. • Mnunuzi atatoa bei ya kununulia pamba kwa WAKALA. • MNUNUZI halazimiki kupokea pamba ilyochini ya kiwango cha ubora kama inavyotakiwa na mamlaka inayosimamia ubora wa pamba. • MNUNUZI atasafirisha pamba ilyonunuliwa na WAKALA toka chama cha msingi hadi kiwandani.

  32. WAKALA. • Wakala atatoa ghala lake litumike kununua pamba kwenye chama cha msingi kwa kipndi chote cha ununuzi • Wakala atatumia wafanyakazi wake na Halmashauri waliopo kwenye chama cha msingi kununua pamba ya -----------. • Wakala atumia mizani na cash box zake. • Wakala atatakiwa kutunza kumbukumbu zote za manunuzi ya pamba. Kumbukumbu hizi zinatakiwa kuandaliwa vizuri na kuwa wazi wakati wote kwa ajili ya ukaguzi endapo zitahitjika. • Wakala atalazimka kuweka ulinzi madhubuti wa mali iliyo ndani y ghala wakati wote wa msimu. • Wakala atalazimika kusindikiza pamba yake inaposafirishwa na mnunuzi kutoka gulioni hadi kiwandani • Wakala atatakiwa kutumia fedha za ununuzi wa pamba kwa kazi iliyokusudiwa tu(ununuzi wa pamba ) na si vinginevyo.Pia wakala haruhusisiwi kuhamisha pamba iliyonunuliwa kwa mnunuzi mwingine. • Wakala hatatoa ghala alilotoa kwa ---------litumke kwa kampuni kununulia pamba au kwa matumizi mengine. • Endapo patakuwepo wa mali au fedha ya mnunuzi Wakala (WATUMISHI PAMOJA NA HALMASHAURI) watawajibika na wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. • Makubaliano haya yamefanywa na wawakilishi wa panned zote mbili leo tarehe---------mwezi--------mwaka--------. • Kny. Kampuni ya ----------------------- • JINA---------------------------------------------------------------------- • SAINI--------------------------------------------------------------------- • CHEO--------------------------------------------------------------------- • JINA-------------------------------------------------------------------- • SAINI------------------------------------------------------------------------ • CHEO---------------------------------------------------------------- • Kny.CHAMA CHA MSINGI • JINA---------------------------------------- • SAINI----------------------------------------- • CHEO--------------------------------------------- • JINA------------------------------------------------ • SAINI----------------------------------------------------- • CHEO-------------------------------------------------------------- • UTHIBITISHO WA AFISA USHIRIKA WA WILAYA. • JINA------------------------------------------------------- • SAINI------------------------------------------------------------------ • MKATABA HUU UMEFUNGWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI HII NA KUTHIBITISHWA NA MAHAMKAMA YA HAKIMU MFAWIDHI WA WILAYA YA ----------------------- • JINA-------------------------------------------------SAINI---------------------- • MUHURI. (HAKIMU MFAWIDHI)

More Related